Header

Carlo Ancelotti kurejea Santiago Bernabeu

Hatimae robo fainali ya michuano ya Klabu Bingwa ulaya imewekwa hadharani,baada ya timu 8 kufuzu sasa zitapambana wiki ya tarehe 10 April ili kutafuta timu zitakazocheza nusu fainali ya champions league .

 Mabingwa watetezi wa ligi kuu Uingereza timu ya Leicester City baada ya kuwatoa Valencia sasa watapambana na Atletico Madrid,Athletico wana njaa na ubingwa safari hii baada ya kupoteza fainali iliyopita ya Champions League.

Leicester hii sio mara yao ya kwanza kukutana na Atletico kwani wameshakutana mara mbili hapo kabla ikiwa ni mwaka 1962 na 1998 huku Leicester akipoteza michezo yote miwili.

 Miamba ya Ujerumani Borussia Dortmund nao watakuwa wenyeji wa Monaco ambao waliitoa Man City katika mechi za 16 bora.Dortmund wenyewe walifudhu katika hatua hii baada ya kuwatupa nje klabu ya Benfica ya Ureno.
Mechi kali itakayovuta hisia za watu ni kati ya mabingwa wa Ujerumani klabu ya Bayern Munich ambao watacheza dhidi ya mabingwa wa Ulaya klabu ya Real Madrid.
https://youtu.be/N-mNJlzDN-M

Comments

comments

You may also like ...