Header

‘Kuwa na Wema imeniongezea vitu vingi vizuri,imenipa heshima pia’ – Calisah.

Kwenye couples ambazo hazikudumu sana na zilienda viral zaidi dakika za mwisho kabla ya kuachana ipo na hii ya Wema Sepetuna Model wa video’s na matangazo Kalisah ambaye kashaonekana kwenye matangazo kadhaa ya Barabarani(Billboards).

Kwenye interview yake na Clouds FM,Calisah amekubali kuwa uwepo wake na Wema Sepetu mapenzini umempa mambo mengi ambayo hakuwahi kuwa nayo>>’Kuwa na Wema imeniongezea vitu vingi vizuri,kuna nyota fulani nilikua sina nimemegewa yaani hata robo’

‘Maisha yangu yamekua mepesi kidogo kwa kuwa nae kwa sababu kila mtu aliyekua anamjua Wema mimi pia alikua ananijua,Nimepata heshima nimepata mlolongo mwingi wa kazi kuwa na mteremko,kuna mengi mazuri nashukuru kwa uwepo wake,kwa sasa tunaongea lakini tuna miezi kama miwili hatujaongea’ – Calisah.

Comments

comments

You may also like ...