Header

Guardian Angel atoa sababu za kusitisha kolabo ndani ya miaka miwili

Muimbaji wa muziki wa injili toka nchini Kenya Aufaxiad Peter a.k.a Guadian Angel ametoa sababu za kwanini amesitisha kazi za kushirikiana na wasanii wenzake kwa muda wa miaka miwili.

Akipiga stories na Dizzim Online amesema kuwa collabos ambazo amekuwa akifanya nyimbo na wasanii wengi zikiwa ndani ya project ya SEVEN HEAVEN iliyoakuwa na maana ya kufanya nyimbo saba ndani ya miezi saba na collabos saba kiasi ambacho mashabiki walianza kulalamika jambo ambalo lilionesha wazi kuwa mashabiki wamekuwa wakishindwa kufocus zaidi kwake.

Hata hivyo amesema kuwa maamuzi ya yeye kusitisha kolabo itamuongezea focus kutoka kwa mashabiki wake ambao wanataka kupata muziki mzuri kutoka kwake kila atakapo kuwa tayari kuachia kazi.

“…nikizidi kujihusisha na mambo ya collbo pia itaweza kunidrain kwasabu ninatumia energy mingi kuweza kupush other projects and push my own projects…sasa pia nichukue muda kufanya vitu vyangu mimi mwenyewe na kuweza kuwafanya watu kufocus kwenye projects zangu mimi mwenyewe…” Alisema Guardian Angel.

Guardian Angek kwasasa anatamba na kazi aliyoshirikishwa na Weezdom inayokwenda kwa jina BETTER MAN iliyotoka mwanzoni mwa mwezi wa pili mwaka huu.

Comments

comments

You may also like ...