Header

‘Kolabo yangu na Boneye wa Kenya tuliipanga miaka 7 iliyopita’ – Joh Makini.

Kwenye kolabo zilizotoka mwaka huu alizoshirikishwa Mwamba wa Kaskazini Joh Makini hii inaweza kuwa ya kwanza kushirikishwa na mshkaji wetu kutoka Kenya aitwae Boneye.

Kitu unachotakiwa kujua ni kuwa kolabo hii imepangwa kufanyika miaka 7 iliyopita lakin haikufanikiwa mpaka mwaka huu 2017 ndiyo imewezekana,Kwenye singo hiyo ya Appetite kashirikishwa pia Konkodi na Owuor Arunga,upande wa Joh Makini amezungumza na kusema >>’Nilikutana na P Unity miaka 7 iliyopita,kipindi ambacho wasanii walikua wanakuja sana Bongo’

‘Mshkaji wangu alikua Nonini ndiye aliyeniunganisha na Boneye kwa sababu ni watu walio kwenye crew moja kwa hiyo tulipanga kufanya kazi,katikati hapo kuna miaka mingi sana imepita ni watu ambao tulipanga kufanya vitu kitambo’

‘Nawaheshimu kwa kitu ambacho wanafanya kwa sababu wamekuwepo kwenye game kitambo sana kwa hivyo waliponiomba kufanya wimbo ule sikuwa na kipingamizi kabisa,kumbuka Arusha na Nairobi ni kama Dar na Morogoro hivyo tunawasiliana sana’.-Joh Makini.

Comments

comments

You may also like ...