Header

Kama wewe ni Mzazi usipitwe na ushauri huu wa Irene Uwoya

Malkia wa Bongo Movie lrene Uwoya haishiwi kutoa ushauri kwa wasanii wenzake au hata watu wanaofuatilia kazi zake na awamu hii amewajia juu wazazi ambao wamekuwa na desturi za kuwachagulia watoto wao kazi za kufanya au fani ya kusomea.

Irene Uwoya amesema kuwa wazazi wanatakiwa waangalie watoto wao wanakipaji gani au wanapenda kusomea vitu gani ili waweze kuwaendeleza katika vitu hivyo na sio kuwalazimisha wafuate matakwa yao.

Watanzania wengi tunapenda kuiga hatutaki kumwangalia mtoto anakipaji gani anapenda nini tunataka tu labda awe dokta awe sijui mwanasheria wakati kipaji hicho hana au hayuko interested na hivyo vitu tofauti na wenzetu nje ,unapomjua mtoto mapema anapenda kitu gani nivyema ukamuendeleza kwenye hicho kwasababu unaweza kupoteza muda wako kwenye kumsomesha ukapoteza tu hela mwisho wa siku isimsaidie japokua elimu muhimu ila elimu imegawanyika kama anapenda elimu ya mpira kuna elimu ya mpira kwahiyo ni vyema kufata anachokipenda ” Amesema Irene Uwoya kwenye Interview na Ayo Tv.

Comments

comments

You may also like ...