Header

Mchekeshaji Kevin Hart apewa heshima kubwa kwenye mji wake

Mchekeshaji na muigizaji maarufu duniani Kevin Hart apewa heshima katika jiji alilokulia la Philadelphia kutokana na mchango wake kupitia tasnia ya uchekeshaji.

Alhamisi hii diwani wa halmashauri ya jiji hilo David Oh amepitisha heshima kwa kutangaza uwepo wa siku maalum ya “Kevin Hart Day” jijini hapo ambayo itakuwa Julai 6, siku ambayo ni kazaliwa Kevin Hart.

Oh,katika kutoa heshima hiyo amesema yeye ameanzisha na kutangaza azimio hilo kama njia rahisi ya kuonyesha shukrani za dhati kwa Hart kwa kuwa balozi mzuri kwa Jiji la Philadelphia.

“…kupitia njia na akili zake za ucheshi wa hali ya juu au kwa njia ya ukarimu wake wa dhati kwa mji wake, Kevin Hart anajua jinsi ya kuleta tabasamu kwa kila mtu katika mji wake wa Philadelphia…” Alisema Oh.

Hata hivyo Hart amefanya kazi ya kurudisha mafanikio yake katika jamii yake,hasa kwa njia ya michango ambapo mwaka 2013 alichangia shilingi $ 250,000 kwenye shule ya kompyuta ya Philadelphia kisha mwaka 2015 alichangia $ 50,000 katika udhamini wa masomo Phildadelphia kwa wanafunzi wa shule ya sekondari akishirikiana na chuo cha Umoja wa watu weusi United Negro College Fund.

Comments

comments

You may also like ...