Header

Pluijm asaini mkataba wa kuinoa Singida United

Baada ya kukanusha habari ya kusaini mkataba na Singida United na picha kusambaa zikimuinesha kocha wa zamani wa Yanga Hans van der Pluijm akiwa na mchezaji mpya (Kutinyu) aliyesajiliwa na Singida United, hatimaye leo March 17, 2017 kocha huyo amesaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo ya mkoa wa Singida iliyopanda kucheza ligi kuu msimu ujao.

Uongozi wa Singida United umetoa taarifa rasmi kwa umma kuthibitisha kumsainisha kocha huyo mkataba wa miaka miwili kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

 

Comments

comments

You may also like ...