Header

Rapa Squeezer aikataa Bongo Fleva

 

Rapa na hitmaker wa wimbo wa NAJA aliomshirikisha ‘Juma Nature’ ambaye kwasasa anaweza kuheshimika kama mkongwe katika muziki wa Bongo fleva Squeezer amesema hayuko tayari kwenda na hali ya muziki ilivyo sasa.

Akizungumza na Planet Bongo ya East Africa Radio Sqeezer amesema kuwa Kipindi kile yeye na wenzake wakati wanatoka muziki ulihitaji kipaji tofauti na sasa ambapo mtu bila kipaji mtu anaweza kuchezesha hela na ukapata hela jambo ambalo mtu hasiyejua kabisa anaweza kufanya biashara ya muziki.

“…sisi kipindi kile tunatoka muziki ulihitaji sana kipaji tofauti na sasa mtu kuchezesha hela na kutengeneza hela…” Alisema Squeezer.

Akikazia kuhusu tafsiri ya yeye kwenye muziki wasasa amesema sio wengi watadumu bali muziki wa watu wasio na vipaji watasikika na wataisha haraka sana.

Hata hivyo Squeezer alisisitiza kuwa lazima msanii awe na knowledge ndo mtu aweze kufanya kitu cha kudumu kwenye game la bongo fleva.

Comments

comments

You may also like ...