Header

Yanga yafanyiwa figisu figisu nchini Zambia

Klabu ya Zanaco FC inataka kutumia uwanja wa taifa wa zambia ‘Mashujaa’ jijini Lusaka kwa ajili ya mchezo wa hatua ya 32 bora ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Yanga,jumamosi hii.

Image result for mashujaa stadium zambia

  Uwanja wa Taifa wa Zambia (Mashujaa Stadium)

Mabingwa hao wa Zambia wanajiandaa kutumia uwanja huo unaochukua mashabiki elfu 60,uwanja huo hivi karibu ulitumika kwenye fainali ya michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ambapo zambia waliibuka kidedea kwa ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Senegal.

“Bado haijathibitishwa rasmi kwani kuna majadiliano na viongozi wa uwanja juu ya kutumia uwanja huo”Amesema kocha mkuu wa Zanaco Numba Munamba.

Mpaka sasa bado hawajatoa sababu yoyote ya kuhamisha mchezo huo na kuupeleka ‘Mashujaa’ vyanzo vyetu nyeti vya habari vinasema huenda ikawa ni figisu figisu za Zanaco kutaka ushindi dhidi ya Yanga.

Comments

comments

You may also like ...