Header

AKA amtambia tena rapper mwenzake Cassper Nyovest

Rapa toka Afrika Kusini AKA ngoma yake ya ‘World Is Yours’ imechukua nafasi ya kwanza katika store ya kuuza muziki ya iTunes  akimpiku aliyekuwa mpinzani wake mkubwa Cassper Nyovest.

Kapitia ukurasa wake wa tweeter Supa Mega AKA aliambatanisha screenshot ya iTunes ukionyesha Cassper na wimbo wake Tito Mboweni kwenye nafasi ya tatu na kusema kuwa hakujua ingeweza kuwa rahisi yeye kurejea kwenye nafasi yake ya juu.

Alitweet “Naam vizuri vizuri …. wakati nilisema, ‘siku zote ningependa kuwa juu tena’ … Sikudhani itakuwa rahisi. ”

Cassper Baada ya kuacha Tito Mboweni, ambayo ilifanya vizuri na kuwa katika nafasi ya juu muda wa dakika 20 baadae Cassper alianza kutweet kuhusu ukubwa wa wimbo na muziki wake huku akiongeza kusema kuwa hakukuwa na ujanja ujanja wowote wa kiabishara ndo aweze kupata attention kubwa ya watu maneno yaliyoonekana wazi kurushwa kwa AKA.

Hali hiyo ya maneno na choko choko kati ya Cassper na AKA walijikuta wanaingia katika mdahalo mkubwa wa muziki wa nani ni bora zaidi.

Cassper aliendelea kusema kwa mashabiki wake kuwa mfalme yeye kama amfalme amerudi. Hata hivyo, AKA alijibu kuwa haiwezi kuwa kupitia maoni ya mtandaoni.

AKA Yeye aliwaambia mashabiki kwamba namba moja kwenye iTunes haaiamui muziki wa nani ni bora zaidi na kuongeza kuwa yeye yuko na furaha ya watu kufurahia vibes ya muziki wake akiwa kwenye #1 au hata awe katika nafasi #10″ kupitia ukurasa wa tweeter.

AKA aliendelea kwa kusema wimbo wake wa “World Is Yours umetoka Desemba. mwezi Machi sasa. Inathibitisha kwamba watu watakutuza kama wewe kama utachukua muda wa kuwapa muziki kubwa na mzuri. ”

Pia AKA alitumia fursa hiyo kuwaambia mashabiki kuwa ataachia albamu mbili, na moja ya kwanza kuja “hivi karibuni”

Comments

comments

You may also like ...