Header

Avril afunguka kuhusu mahusiano na Dennis Oliech.

Muigizaji na mwanamuziki toka nchini Kenya Judith Nyambura Mwangi a.k.a Avril amezungumzia mahusiano na uvumi uliozagaa kuwa anatoka kimapenzi na mchezaji wa mpira wa miguu wa timu ya taifa Harambee Stars Dennis Oliech.

Wawili hao tetesi zimezagaa kutokana na wao kuonekana pamoja mara kadhaa pindi tu baada ya kuvunjika kwa mahusiano ya Avril na mapenziwe wa zamani toka Afrika Kusini Leslie Mugadza.

“siko katika mahusiano ya kimapenzi na Dennis. Ni moja ya marafiki zangu wakubwa tangu zamani. Tumekuwa marafiki kwa muda wa miaka sita sasa. Namjua hata kabla nikutane na aliyekuwa mpenzi wangu na mara kwa mara tunakuwa pamoja” alisema Avril na kuendelea kusisitiza kuwa anawasiliana nae kama rafiki.

“tuko vizuri sana,tunaongea,tunawasiliana mara moja moja na mimi sio aina ya watu ambao uwasema vibaya kwa maneno yasiyo ya kweli. Kama watu wengine,tunaachana na maisha yanaendelea” Alisema Avril.

Comments

comments

You may also like ...