Header

Drake aweka rekodi mpya kwenye mtandao wa Spotify

Ukitaja wasanii wenye mafanikio kwenye muziki huwezi acha kulitaja jina la Drake kwani mbali ya mauzo ya kazi zake msanii huyo pia amechukua karibia tuzo kubwa zote duniani na kuweka rekodi chungu nzima na awamu hii ameweka rekodi kwenye mtandao wa spotify.

Mtandao wa Forbes umetoa taarifa kuwa Drake ndie msanii pekee na wa kwanza kufikisha Streams Billioni 10 kwenye mtandao wa Spotify, nafasi kubwa ya kujipatia namba hizo zote zimetokana na Album yake ya Views ambapo nyimbo kama “One Dance” yenyewe imefikisha zaidi ya wasikilizaji bilioni moja.

Hiyo inaweza kuwa ni habari nzuri sana kwa mashabiki wa Drake kwani wakati wanasherehekea namba hizo, pia mashabiki wakae mkao wa kula kwa ujio mpya wa Project yake ya “More Life” ambayo inatarajiwa kuachiwa leo jumamosi tarehe 18/3/2017.

Comments

comments

You may also like ...