Header

Joh Makini tulishazungumza kuhusu kufanya kazi – Chid Benz.

Rapa wa muziki wa kizazi kipya cha Bongo Fleva Rashid Makwiro a.k.a Chid Benz amefunguka sababu za yeye kushiriki kolabo na rapa mwenzake Joh Makini.

Akizungumza na Dizzim Online Chid amesema kuwa yeye hana tatizo  na Joh hivyo wanachoweza kufanya kwa pamoja ni muziki.

“…kuna siku moja tulikuwa tunazunguka kwenye tour flani mimi nilikuwa nasikika na beat nilikuwa naipiga chumbani kwangu hotel kila siku Joh Makini siku moja alikuja akaisikiliza ile beat akasema ahaa… chuma hii beat kali sana itabidi tufanye kitu nikamwambia yaaah tukirudi Dar usijali tutacheckiana tutarecord tulivyorudi Dar mimi sikupata nasafi tena ya kumcheck Joh…ninavyoona inawezekana tukaja kufanya kazi kwasababu yeye ni msanii mimi ni msanii…hatuna maneno mimi nayeye nayeye…” Alisema Chi Benz.

Hata hivyo mbali na Chid Benz kusema kuwa yuko tayari kufanya kazi na Joh Makini habari nyingi zilizowahusu wawili hao ni kuonekana kama wasingeweza kupika chungu kimoja.

Comments

comments

You may also like ...