Header

Malimu Busungu kusalia Jangwani

Mshambuliaji wa Yanga Malimu Busungu ambaye amecheza dakika 30 tu kwa msimu huu wa ligi kuu Tanzania bara lakini bado nyota yake inaonekana kung’ara kwa wanajangwani baada ya kuanza mazungumzo ya mkataba na mchezaji huyo.

Akiongea na DizzmOnline meneja wa mchezaji huyo Yahaya Tastolo amesema kuwa anaendelea kupokea ofa mbalimbali kuhusu Busungu lakini Yanga wao wameonesha nia ya kuongeza mkataba.

Angalau kwa sasa Busungu ameanza kurejea kwenye hali ya mchezo kwani Busungu sio mchezaji mbaya ila kuna mambo yalitokea kumuondoa mchezoni jambo ambalo wataalam wa soka huwa tunaamini ni jukumu la kocha kumuweka sawa mchezaji“Amesema Yahaya Tastolo.

 

Comments

comments

You may also like ...