Header

‘Barakah ni ngumu kumuuza kulingana na intertainment ilivyojijenga’ Management.

Kama ni msomaji wa maoni au comment mbalimbali za kwenye mitandao ya kijamii utakua umeziona baadhi ya comment zikidai kuwa muziki wa Alikiba umeumeza muziki wa Barakah kiasi cha kumfanya Barakah ashindwe kuonekana kwenye muziki wake na anaonekana kama chawa (shabiki) wa Alikiba.

Seven Meneja wa Alikiba na Barakah.

Jambo hili pia lilishawafikia uongozi wa Alikiba na walikua wanasubiri siku ya kulitolea ufafanuzi,kwenye sentensi zake Meneja wa Rockstar 4000 Seven Mosha amesema>>’Ni utaratibu ambao watu wameshazoea au sababu hamna Records label nyingi Tanzania ni kama wewe ni Simba au Yanga’

‘kwa Barakah inakua ngumu hata kwake kumuuza kwa sababu intertainment ilivyojijenga sasa hivi lakini ni kitu kigeni kwa sababu RockStar haijasaini wasanii wengi kwa hiyo kwa wale wasanii wachache inaonekana kama wako chini ya mwamvuli wa Kiba,lakini tunavyoendelea mbele watu wanaanza kuelewa jinsi ya kutofautisha vitu’.

Gabo Zigamba asema udhaifu wa Bongo Movie ndiyo uliomfanya ang’are mtazame hapa chini kwa kubonyeza play

Comments

comments

You may also like ...