Header

Baada ya Big Brother,Hili ndilo shavu lingine alilolipata Idris Sultani nje ya Tanzania.

Shindano la Big Borther Africa mwaka 2014 lilimtangaza Idris Sultan kama mshindi wa mwaka huo,ambapo kiasi kilichotangazwa kwa mshindi ni kupatiwa dolar za Kimarekani 300,000 ambayo kwa pesa za Kibongo zilikua zaidi ya Milioni 500.

Ukiachana na stori hiyo, Idris baadae aliingia kwenye headlines ya kutoka kimapenzi na Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu,kwa sasa Idris yuko na taarifa njema kama hukua ukifahamu ni kuwa Idris ameingia pia kwenye filamu na moja kati ya filamu anaoonekana ni pamoja na Kiumeni ambayo imezinduliwa siku chache zilizopita na baada ya kuzinduliwa tayari kuna deals Idris kaanza kupata.

Kwenye Red Carpet ya Mliman City siku ya uzinduzi wa filamu hii Idris amesema tayari kuna nchi mbili ameshapokea mualiko wa kwenda kufanya kazi>>’Nina movie kama mbili kuna moja iko Rwanda nyingine South Africa,mitonyo sitaki kusema ukishasema mitonyo sasa unaanza kuvuta wadada wa tofauti kidogo na wale unaowahitaji wewe’

‘Waliongea na Madirector wakasema tumeona clips kadhaa za movie zako na ni movie za English by the way nikatumiwa script nikaangalia character nikaona ni tamu nikachukua kama wiki kumaliza script,nyingine sijaconfirm kwa sababu kuna mabadiliko yanafanyika bora kuwaambia Watanzania vitu vikiwa vimekamilika kuliko kusema naenda kufanya movie South halafu wanashangaa miaka miwili,miaka mitatu halafu wanaanza kuuliza ile movie ya South vipi,sitaki kusema hivyo’.

Unaweza kubonyeza play kumtazama Idris wakati akitoa ufafanuzi kuhusu deal hili alilolipata nje ya Tanzania na namna alivyopania kutia mguu kwenye soko la Hollywood.

Comments

comments

You may also like ...