Header

Yaya Touré ampigia upatu Pep Guardiola

Mchezaji wa Man City Yaya Toure ambaye mwanzoni mwa msimu alikuwa njia panda kusalia/kuhama klabuni hapo kutokana na matatizo baina yake na kocha wa timu hiyo Pep Guardiola sasa tofauti zao zimekwisha na ameendelea kumpigia ubatu kwa watu wanaombeza Pep kwa kushindwa kuivusha klabu hiyo kwenye michuano ya UEFA na kutolewa na Monaco.

Toure anaamini aina ya uchezaji wa Manchester City utawapa makombe mengi tofauti na watu wanavyofikiria “ukiangalia jinsi tunavyocheza na mbinu za mwalimu naamini inaweza kutuletea makombe,hata kama sio msimu huu lakini mbeleni tutapata.”

Kuhusu kupingwa kwa mbinu za Guardiola, Yaya anasema “huwezi ukakwepa wapingaji,sio kila kitu kinakubalika kwa kila mtu na inapaswa uwe tayari kwa hilo,najua watu wanasubiri tufeli lakini sisi haitupaswi kuangalia hivyo bali tufanye kazi kwa bidii sana”

Yaya Toure anasema wao kama Man City hawasikii kelele za watu wengine bali wanapambana tu,ameongezea kuwa timu yao inafurahia mfumo wa kocha wao na wala hawana mpango wa kubadilisha aina yao ya uchezaji.

Toka Pep Guardiola ajiunge na Man City akitokea Bayern Munich, maneno na upinzani umekuwa mkubwa juu yake. Wengi wamekuwa wakipinga aina yake ya uchezaji wakidai inawafanya Man City waonekane wa kawaida sana,kutolewa katika Champions League kumeleta kelele nyingi zaidi lakini Toure bado anamkubali Pep.

Comments

comments

You may also like ...