Header

Arsenal yaichapa Tottenham goli 10-0

Mabingwa watetezi wa Kombe la FA Uingereza upande wa wawanawake Kina dada wa Arsenal waliwalaza wapinzani wao Tottenham 10-0 na kufika robo fainali Jumapili.

Danielle van de Donk alifungia wenyeji hao mabao matatu, naye mshambuliaji wa zamani wa Sunderland Beth Mead akafunga bao pia mechi yake ya kwanza kuchezea Arsenal.

Chelsea, ambao walishindwa na Arsenal fainali mwaka jana, pia walipata ushindi mkubwa, kwa kulaza Doncaster 7-0.

Bristol City walilaza Millwall 5-0.

Liverpool, Notts County, Birmingham na Sunderland pia walishinda kwenye mechi hizo za raundi ya tano.

Droo ya robofainali itafanyika baadaye Jumatatu.

Matokeo kamili mengine ni Manchester City 1-0 Reading (Jumamosi),Arsenal 10-0 Tottenham,Birmingham 2-0 West Brom,Bristol City 5-0 Millwall,Chelsea 7-0 Doncaster,Liverpool 2-1 (AET) Everton,Notts County 3-2 Yeovil,Sunderland 3-2 Aston Villa.

CHANZO: MTANDAO WA BBC

Comments

comments

You may also like ...