Header

Hawa ndiyo marapa waliomshawishi Country Boy kuingia kwenye muziki

Rapa kutoka Tanzania Country Boy anayefanya poa na wimbo wake Hakuna Matata aliomshirikisha Billnass ametaja kiazi ambayo wadau wangemtambua nacho kama asinge kuwa msanii wa muziki.

Akizungumza kupitia XXL ya Clouds Fm amesema kuwa alikuwa ni mchezaji mzuri wa mpira wa miguu na akusimulia kisa cha yeye kuachana na mpira kuingia kwenye muziki na kuwataja baadhi ya marapa waliomshawishi kwa kiasi kikucha cha yeye kuendelea kufanya muziki mpaka sasa.

“sana sana mpira ni kitu ambacho nakiweza sana…sikuendelea nao unajua jinsi ambavyo nilivyokua katika mazingira mazingira yangu mi yalikuwa magumu kidogo katika upande wa mpira…walikuwa wakiondoka nakariri mistari yao nachana naenda shule na mimi naimba  nimeshafanya show zangu za shule huko kupitia nyimbo za mabrother …kwa hiyo ile ikanijenga mimi nikajikuta na mimi nasema let me try…let me try” Alisema Country Boy.

Hata hivyo Country amewata Babuu,Langa,Chid Benz,Ngwear, Soggy Dogg, Professor Jay na Kurasa miongoni mwa wasanii waliomshawishi.

Comments

comments

You may also like ...