Header

Je,Harmonize kamuimbia Wolper wimbo wake mpya wa ‘NIAMBIE’? Na alimlipa Shilingi ngapi kuonekana kwenye Video yake? majibu haya hapa

Msanii kutoka lebo ya muziki inayofanya vizuri kwa sasa katika muziki wa Tanzania WCB, Harmonize amesema kuwa wimbo wake mpya wa Niambie hakuandika kwa lengo la kumfikishia ujumbe Jackline Wolper ambaye ni Mpenzi wake kama ilivyokuwa ikielezwa katika mitandao ya kijamii na vijiwe tofauti tofauti hapa Bongo.

Kupitia kipindi cha The Playlist cha Times Fm Harmonize amesema moja kati ya sababu ambazo zilifanya aandike wimbo huo ni kwa sababu ya Uzuri pamoja na umaarufu alionao Wolper amweleze kama atakuwa nae kwa kipindi chote, lakini pia ni stori ambayo mshikaji wake pia alimueleza.

Wakati naanza Kudate na Jack, Jack ameanza kuwa maarufu kabla yangu,usafiri wangu mimi ulikuwa bajaji tu,sometimes alikuwa ananifuata, isitoshe Jack ni mwanamke mzuri so wanaume wengi watakuwa wanamtaka na nini, lakini sikuishia hapo tu, kuna mwanangu mwingine nae alinipa story kama hii,so nikaona Idea ni nzuri na nikiifanya watu wengi wataipenda na nikaona nifanye na Jack kwa sababu Ni mwanamke wangu lakini pia nikaona itakuwa hamasa kwa watu wengi zaidi kupenda wimbo huu kwa kuusikiliza na kuutazama pia” Alisema Harmonize

Aidha akieleza kuhusiana na malipo katika sehemu alizotokea Jack kwenye Video ya wimbo wake wa Niambie Harmonize amesema kuwa hakutoa Pesa yeyote ile kwa Wolper kwa ajili ya malipo kama Video Queen kwenye Wimbo wa Niambie.

Sikumlipa Wolper, katika wimbo wangu wa Niambie, Jack ni Mwanafamilia, na sisi huwa tunasaidiana katika kazi mbalimbali, nikimsaidia leo na yeye atanisaidia kesho katika jambo lolote ambalo nitataka kulifanya” aliongeza Harmonize.

Comments

comments

You may also like ...