Header

‘Pesa ya Madafu imerudisha heshima kwa wakongwe’ – JAY MOE

Rapa mkongwe wa hip hip Bongo ‘Jay Moe’ ameweka wazi kilichomfanya yeye kufanya video kali ya ‘Pesa ya Madafu’ ni ili kuwathibitishia uwezo wake kwa wale waliokuwa wakimsema kuwa hana uwezo wa kutengeneza kazi nzuri.

Akiongea na East Africa Radio kwenye kipindi cha Planet Bongo Jay Moe amesema kuwa vijana wa sasa wengi wana mawazo ya kwamba wakongwe waliopo kwenye ‘game’ ya bongo hawana uwezo wa kutengeneza video ambazo zinaweza kupendwa na watu wengi kama wafanyavyo wasanii wa sasa.

“Zamani sisi tulikuwa tunashindana kuandika mistari, tunamtafuta mkali wa mashahiri, hiki kizazi cha video kali kilipokuja wakaanza kutudharau wakongwe kuwa hatuna uwezo wa kufanya kama wao lakini dharau zikazidi kuwa wasanii wa ‘generation’ yangu hatuna pesa ndipo nikaamua kutengeneza kichupa cha pesa ya madafu kikali kuwa- ‘prove wrong”. Alisema Jay Moe.

Pamoja na hayo Jay Moe ameelezea kilichokuwa kikimfanya miaka ya nyuma kushindwa kufanya video nzuri kuwa ni kwa sababu alikuwa chini ya lebo (Bongo Record) hivyo bajeti zote alikuwa akipangiwa tofauti na sasa ambapo anajisimamia mwenyewe.

“Ukiwa chini ya uongozi kila kitu unapangiwa, kwa hiyo hata bajeti nilikuwa napangiwa, mwaka 2010 niliwaambia wenzangu mimi najipanga kwanza na maisha sitaki kuja kuaibika baadaye kwa kutokuwa na maendeleo, sasa hivi hata ukiniona sipigi show lakini nina uwezo wa kwenda kufanya video South kesho kwa sababu ya uwekezaji niliokimbilia kuufanya kipindi nipo kimya”. Jay Moe.

Comments

comments

You may also like ...