Header

Drake awa msanii wa kwanza kuwa na streams bilioni 10 kwenye Spotify

Drake ameendelea kuvunja rekodi nyingi kwenye muziki wa Marekani. Rapper huyo ambaye Jumamosi aliachia album yake mpya, More Life, amekuwa msanii wa kwanza kuwa na streams bilioni 10 kwenye mtandao wa Spotify.

Sehemu kubwa ya mafanikio hayo, imetoka kwenye album yake Views iliyotoka mwaka jana ikiwa na hits kama ‘One Dance’, ambayo ilivutia streams bilioni 1.15.

Kutoka kwenye albamu hiyo, wimbo wake Hotline Bling umechezwa kwa zaidi ya mara milioni 600, Too Good milioni 520 na Controlla mara milioni 340. Kwa jumla, nyimbo kutoka kwenye album ya Views zimesikilizwa kwa mara bilioni mbili.

Comments

comments

You may also like ...