Header

“Kama unataka kiki dunia ikujue panda dau” – Shilole

Hitmaker wa ngoma Sitoi kiki kutoka katika muziki bongo Zena Yusuf Mohammed a.k.a Shilole atoa njia rahisi ya kibiashara(kiki) kwa yeyote atakaye hitaji jina lake.

Akizugumza kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio kuhusu swali asilopenda kuulizwa ni pamoja na mahusiano yake yaliyopita kwa kuwa yeye kujibu swali la namna hiyo ni kutoa kiki bali kwasasa kiki yake inatoka kibishara tu.

“ndo maana sitaki kutoa kiki mwanagu au unataka nitoe kiki yaani hii ukiniuliza mi natoa kiki sahivi nimegoma kutoa kiki mwanagu kiki tunasaini…Shishi nataka kiki mwanagu dunia inijue me i don’t care tunasaini milioni hamsini hapa unaweka mezani tunatoa kiki” Alisema Shilole.

Hata hivyo Shilole amesema tangu kuachana kwake na mpenziwake hajaingia katika mahusiano yoyote mapya.

 

 

Comments

comments

You may also like ...