Header

Tammy The Baddest aguswa na #WasafiDotCom ya Diamond Platnumz

Msanii wa Hip Hop kutoka Tanzania Tammy the baddest amemuunga mkono Diamond Platnumz kwa kufungua mtandao wake wa Wasafi Dot Com kama jitihada za kuukomboa muziki wetu wa Bongo Fleva.

Akiongea na DizzimOnline Tammy amesema kuwa anaheshimu kitu ambacho Diamond amekifanya kwenye muziki huu wa Tanzania kwani ameupa heshima kubwa na kuutambulisha kimataifa lakini kubwa zaidi ni hii platform ya Wasafi dot com ambayo ameileta kama mkombozi ya vilio vya wasanii wengi kuhusu kupotea kwa mapato ya kazi zao mitandaoni.

“Nampenda sana Diamond Kwasababu kautangaza sana Muziki wetu Kafanya vitu vikubwa sana ambavyo wasanii walopita hawakuwahi kufanya ukijalibu kuangalia hii wasafi dot com mimi mwenyewe nimeshawishika kwenda kuweka nyimbo zangu kwasababu naamini nisehemu sahihi na wasanii tumuunge mkono ” Amesema Tammy the Baddest.

Comments

comments

You may also like ...