Header

Kwa maelezo haya hutamsikia tena Shilole akizungumza Kiingereza hadharani

Msanii wa kizazi kipya ‘Shilole’ anayetamba na wimbo wake wa ‘Hatutoi kiki’ amefunguka kuwa hapendi kuzungumza lugha ya Kiingereza pasipo sababu kwakuwa ametumia gharama kuilipia lugha hiyo, na hivyo hakuna wa kumpangia kuizungumza.

Akiongea  East Africa Radio kwenye kipindi cha Planet Bongo Shilole amesema kwamba watu wanaomtaka yeye kuzungumza Kingereza wanapoteza muda wao kwa kuwa yeye alijifunza lugha hiyo kwa ajili ya maslahi yake binafsi hasa katika biashara zake.

“Mimi lugha naijua sana, nimesoma kozi ya miezi mitatu, mwalimu alikuwa anakuja nyumbani kwangu kunifundisha, ukitaka kujua mimi najua kuzungumza lugha hiyo unikute kiwanja cha ndege nimechelewa ndege halafu nina show au ninapokuwa mezani nataka kuzungumza na wazungu kwa ajili ya kusaini mikataba lakini siwezi kuongea kwa kila mtu ili kudhihirisha kama naweza kwakuwa hakuna aliyenisaidia kulipa ada”. Alisema Shilole.

Katika hatua nyingine Shilole amesema amechoka kutumiwa kama daraja la kuwanufaisha watu ambao wanaenda kwake kujipatia umaarufu ili wafanye mambo yao mengine ndiyo sababu ya kuachia wimbo wake mpya ambao ni salamu kwa wale wote wenye mawazo ya kutoka kupitia jina lake.

 

Comments

comments

You may also like ...