Header

Lady Bee aelemewa na muziki wa injili

RAPA wa kike Lady Bee, aliyebadili na kuwa msanii wa injili amesema kuwa anayaona maisha kuwa magumu zaidi ya yalivyokuwa zamani alipokuwa akifanya muziki wa kidunia.

Rapa Lady Bee mmoja wa marapa wa kike wakali kuibuka katika tasnia ya muziki wa Kenya kisha akaingia katika maisha ya ijili mwaka 2012 na mpaka sasa ameachia nyimbo zake mwenyewe na nyingine za kushirikishwa za injili.

Lakini Lady Beee anahisi hatua yake ya kuanza kuishi maisha ya uokovu matokeo yamekuwa tofauti mpaka sasa.

Akifunguka kuhusu maisha yake ya wokovu, Lady Beee amesema, “Safari yangu katika imani haijawa rahisi. Wakati mwingine huwa nahisi ni kama nazama.

“Nahisi ni kama siwezi kusonga tena na maisha yangu ya nyuma yalikuwa mazuri zaidi ya yalivyo kwa sasa. Nahisi ni kama nimeanza kulemewa na safari hii,” alifunguka ila akasisitiza kuwa anaamini Mungu atampa nguvu.

Tangu abadilike, Lady Bee amekuwa akiendesha maisha ya ukimya sana tofauti na zamani ambapo kila siku angeamkia kuzua skendo.

Comments

comments

You may also like ...