Header

Madee akumbuka shuka kumeshakucha ‘wanafungwa kwakusingiziwa kesi’

Kutokana na Mfululizo wa Matukio yanavyoendelea hapa nchini hususani kwenye sakata la Vyombo vya Habari na RC Makonda huenda ikawa ni chanzo cha Rais wa Manzese Rapa Madee kupata funzo la kuamini kuwa kuna watu wanaofungwa kwa kesi za kusingiziwa.

Madee kupitia ukurasa wake wa Twitter mapema baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya kamati ya uchunguzi wa kuvamiwa kwa kituo cha Clouds FM iliyodai kuwa RC Makonda aliwatishia Watangazaji kuwafunga miezi 6 endapo watakataa kurusha kipindi alichotaka kiende hewani.

Rapa madee huenda akahusisha tukio hilo moja kwa moja kwa kutweet “Leo ndio nimegundua wengi wanafungwa kwakusingiziwa kesi!!!” kwani hata hivyo naweza kusema Madee amechelewa kujua hilo kwani tangia zamani LWP Majitu miaka ya Nyuma waliwahi kutunga wimbo wao mkali sana ulioitwa JELA na kwenye wimbo huo kuna mistari inasema Wanaokwenda jela sio wote wana hatia.

Comments

comments

You may also like ...