Header

CHIKUZEE Ndani Ya Wasafi, Kunani?? Details Zaidi Hapa

Msanii mkali wa humu nchini CHIKUZEE ambaye anatokea pande za Mombasani, Kwa sasa yuko nchini Tanzania kwa mitikasi za kimuziki. Mkali huyo wa hitsong ya ‘Ngoma itambae’, hivi majuzi alikuwa kwenye ofisi za WCB jijini Dar er Salaam, Tulimtafuta meneja wake kwa njia ya simu na alitudokezea kwamba kuna mambo mengi wanafanya na label hiyo ya wasafi, mojawapo ikiwemo kuuza Kazi za Chikuzee kupitia wasafi.com, kurecordi nyimbo na wasafi records na pia kuna uwezekano kufanya kazi na msanii mmoja wa Label hiyo inayomilikiwa na Diamond Platnumz .

Meneja huyo wa Chikuzee pia aliongezea kwa kusema kuwa mbali na Wasafi, wanafanya kazi na ma producers wengine nchini Tanzania kama vile MANECK, TOUCH na MANDUGU DIGITAL.

 

Comments

comments

You may also like ...