Header

Harmonize Ajipanga Kuachia Album Baada Ya Diamond

Msanii Harmonize kutokea label ya WCB ambaye sasa hivi anafanya vizuri na nyimbo yake mpya ‘Niambie’, amesema baada ya kiongozi wa label hiyo Diamond Platnumz kutoa album yeye atauomba uongozi wake pia afanye hivyo kwani aliaibika alipofika Marekani alipoulizwa ana album ngapi kama msanii akakosa jibu. “Nadhani Mondi akishamaliza suala la Albamu mimi nitafuata kwa sababu nilipokuwa Texas kuna mdada nilimuambia mimi ni msanii kutoka Tanzania akaniuliza mpaka sasa una albamu ngapi nikashindwa kumjibi, hii ni aibu ukiwa na albamu kadhaa lazima watu wakuheshimu” aliongeza Harmonize.

Comments

comments

You may also like ...