Header

Fid Q atoa sababu za kutojihusisha na masuala ya kisiasa yanayoendelea kwasasa

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na mkongwe wa hip hop kutoka Tanzania Farid Qubanda a.k.a Fid Q ametoa sababu za kwanini hakupost wala kutoa maoni juu ya sakata la kutenguliwa kwa aliyekuwa waziri wa habari, utamaduni sanaa na michezo Tanzania Nape Nnauye.

Akizungumza na Dizzim Online Fid Q amesema kuwa ameamua zaidi kutumia muda mwingi kwenye muziki na sanaa yake pamoja na kutaja kukosa elimu na ujuzi wa siasa kama moja ya sababu zilizomfanya akae kimya.

“mwaka huu nimeamua zaidi kuwa msanii, nimeamua zaidi kuzingatia sanaa yangu na kuachana na vitu ambavyo sivijui…katika vitu ambavyo sivijui ni pamoja na siasa, kwahiyo nilichoamua ni meamua kuwa msanii tu msanii niwe busy tu na sanaa yangu kwahiyo nakosa maoni nakuwa nashindwa kujua nini kinaendelea na vitu kama hivyo” Alisema Fid Q.

Hata hivyo Fid Q amewashauri watanzania kukumbuka kuwa Tanzania ni taifa lenye sifa kuu ya AMANI hivyo haoni sababu za kuipoteza kwa kipindi hiki na kinachokuja.

Comments

comments

You may also like ...