Header

Jonas Mkude ampa mechi mbili kocha wa Taifa Stars

Nahodha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na nahodha wa klabu ya msimbazi Simba Sports Club Jonas Mkude amesema kuwa michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Botswana na Burundi ni kipimo kizuri kwa kocha mkuu Salum Mayanga.

Akizungumza na DizzimOniline Mkude amesema kuwa Mayanga ni kocha mzuri na anaweza kutufikisha mbali kikubwa watanzania na wadau wa soka kumuunga mkono.

“Mimi ninaona hizi mechi mbili ni nzuri sana kwa kocha mkuu Salum Mayanga baada ya kuteuwa kikosi kwa mara kwanza ilikujua wachezaji alioteuwa wakoje  pia zitatusaidia kujiandaa kwa ujumla” Alisema nahodha Jonas Mkude

Taifa Stars itajitupa uwanjani kesho kuminyana na Botswana kwenye dimba la Taifa jijini Dar es salaam kabla ya kucheza na Burundi siku ya jumanne.

Comments

comments

You may also like ...