Header

Kuelekea mchezo wa Taifa Stars vs Botswana: Kocha wa Botswana ‘Peter Butler’ aingiwa hofu

Kocha mkuu wa timu ya taifa Botswana maarufu {The zebras} muingereza Peter Butler ameingiwa hofu juu ya kikosi cha Tanzania Taifa stars baada yakupata muda wakukiona kikosi hicho cha Salum Mayanga.

Akizungumza mbele ya waandishi  wa habari Peter Butler amesema amepata muda mfupi  wa kukiona kikosi cha Stars na amekimwagia sifa kikosi  hicho kuwa kimesheheni vijana na wenye vipaji na kukiri wazi kuwa mchezo wa kesho utakuwa mgumu.

Natarajia kuwa mchezo kesho utakuwa mgumu sana kwa sababu nimegundua kuwa kikosi cha Taifa Stars kina vijana wengi kulinganisha miaka ya iliyopita naamin watatoa ushindani na kufanya  mchezo kuwa  mgumu kwa pande zote mbili”  Alisema kocha mkuu wa Botswana Peter Butler

Taifa stars kesho majira ya saa.10:00 za jioni watavana na Botswana kwenye dimba taifa jijini Dar es salaam kwemye mchezo wa kirafiki na viingilio vitakuwa kama ilivyokuwa hapo chini kwenye jedwali.

Comments

comments

You may also like ...