Header

MC Pili Pili amlilia Kikwete

Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Tanzania MC Pili Pili ni moja kati ya watu ambao wamevutiwa sana na uongozi wa Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ambaye yeye mpaka leo anaamini ndiyo rais wake bora na yupo tayari kumchekesha hata kama kwenye sherehe za Birthday.

Alivyokutana na DizzimOnline MC pili pili alisema katika kufanya kazi kwake kote kwenye maisha yake bado hajawahi kufanya kazi mbele ya Kikwete na bado ana ndoto siku moja kuja kukutana na Mzee Kikwete na kupiga nae japo picha kwani amedai Kikwete alikuwa na sura ya urais.

Msikilize hapa chini akizungumza na DizzimOnline

Comments

comments

You may also like ...