Header

Nape Nnauye aeleza dhumuni la kuitisha mkutano na Waandishi wa habari

Aliyekuwa waziri wa habari, utamaduni sanaa na michezo mheshimiwa Nape Nnauye afafanua mengi kuhusu kilichotokea jana kabla na baada ya utenguzi wa Rais John Pombe Magufuli na kumteua waziri mpya kuziba nefasi yake Mheshimiwa Harrison Mwakyembe.

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya DW amesema kuwa alishaziona dalili za kutenguliwa kwake na sababu kuu iliyompeleka kutaka kuzungumza na waandishi wa habari ilikuwa ni kumpongoza waziri mpya aliyepewa jukumu la nafasi yake na kuwa kuwaomba watanzania watoeushirikiano kwa waziri huyo mpya.

“nilikuwa Arusha nikaamua kurudi Dar es salaam kwasababu mimi ni mwanahabari lazima yangesemwa mengi bila mimi kusema ingekuwa si sawa nikaamua nikiutane na wanahabari kwakweli kimsingi ilikuwa ni kueleza shukrani zangu  kwa Rais kwa kuniamini kwa mwaka, kuwashukuru wadau amabo nimeshirikiana nao lakini kumpongeza waziri mpya wa habari mzima lakini pia kuwataka wadau wamuunge mkono…Dalili zilikuwepo lakini kama ambavyo nilivyoteuliwa sikuambiwa hakukuwa na sababu ya kuniambia wakati anateua mtu mwingine kwasababu kwa taratibu zetu kikatiba hamshauriani “ Alisema Nape.

Hata hivyo zoezi hilo la kuzungumza na waandishi wa habari lilivunjwa na RPC wa kanda maalumu ya Kinondoni jambo ambalo lilizua tafrani kiasi cha Mh. Kutishiwa silaha ya moto katika harakati za kumzuia asizungumze na waandishi arudi kwenye gari.

Zoezi hilo la kumzui Nape halikuwezeknana kwani aliweza kuzungumza kupitia uwazi wa juu wa gari na kuwataka watanzania waliinde amani ya taifa lao kwakuwa yeye ni mkubwa lakini taifa ni kubwa zaidi yake.

 

Comments

comments

You may also like ...