Header

Cristiano Ronaldo apewa uwanja wa ndege Madeira,Ureno

Ukiwa shujaa wenzetu wanakupa heshima na hiki ndicho kilichotokea kwa mshambuliaji nyota wa Real Madrid na timu ya taifa ya ureno  Cristiano Ronaldo kwani Serikali ya kisiwa cha mji wa Madeira nchini Ureno imeamua kubadili jina la Uwanja wake wa Ndege kutoka “Madeira Airport” na kuwa Uwanja wa Ndege wa Cristiano Ronaldo.
Tayari mabadiliko yameanza kufanyika na tarehe 29 March uwanja huo utatangazwa wakati wa uzinduzi rasmi,Ronaldo ni Mreno aliyezaliwa kisiwani humo, kisiwa ambacho kiko karibu na kile cha Hispania kinachomilikiwa na Hispania Cha Tenerife ambacho Mtanzania, Farid Mussa anacheza soka huko.
Ronaldo amekuwa nahodha wa kwanza kuiwezesha Ureno kubeba ubingwa wa Ulaya, mchezaji mwenye mafanikio akiwa England (Manchester United), Hispania na Real Madrid pia amefanikiwa kubeba ubingwa wa Ulaya na kuwa mchezaji bora wa dunia mara nne mfululizo.

Comments

comments

You may also like ...