Header

Mr. T Touch amsaini Young D

Rapa Young David a.k.a Young D amechukua uelekeo mpya na kufuata mfumo mpya wa muziki kwa kumshirikisha Mr T. Touch.

Iko wazi kuwa kwasasa tukizungumzia hit song kutoka Tanzania  ni wengi hawataacha kumtaja Mr. T Touch kwakuwa ameshiriki katika mfululizo wa hits nyingi kupitia studio ya Touch Sound ambayo ni lebo ya muziki pia. Mr. T amebainisha kumsaini Young D na tayari wameshaandaa kazi zipatazo sita chini ya lebo hiyo.

“Mimi nimeingia mkataba mrefu wa miaka mitatu na Young Dee na ataendelea kuwepo chini ya Touch Sound na mimi ndiye nitakayesimamia na kutengeneza biti za nyimbo zake zote na nia yangu ni kumfanya afanye vitu tofauti na alivyokuwa akifanya hapo awali kwa kuwa mimi namuona ni msanii mwenye biashara”  Alisema T. Touch

Hata Young D muda wowote ataachia kazi chini ya lebo ya Touch Sound na yupo msimamizi ambaye atahakikisha kazi zinaenda sawa kwa mujibu wa Mr. T. Touch.

Comments

comments

You may also like ...