Header

Otile Brown wafikishana pabaya na Menejimenti yake

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Mombasa Kenya Otile Brown amesema kuwa muda wowote atalifanyia kazi suala linalo endelea baada ya iliyokuwa menejimenti ya Dreamland Music kuandika mtandaoni kuwa kazi zote zilizofanyika chini ya usimamizi wake haziruhusiwi kutumika katika matamasha au kiabiashara.

Dreamland Music baada ya kutoelewana na Otile brown alipost mtandaoni kuwa kulingana na mkataba wa wawili hao jambo ambalo Otile anadai limemgharimu kiasi cha kupoteza shows zenye thamani kubwa kwa hofu ya waandaaji.

Hata hivo Otile amesema kuwa kilichobaki ni kumfungulia mashtaka Dr. Eddie ambani nide mmiliki wa Record lebo hiyo kwakuwa anadai kinachoendelea ni kukoseana heshima.

“kilichobaki mimi ni kumfungulia mashtaka ambapo mimi sitachukua muda kwasababu ananikosea heshima upande wangu, amenizui show kama tano sasa hivi kwa kile alichokiandika pale kwasababu watu wengine hauwezi kuwaconvice kwamba si kweli watu wengine wanahofia maana ni hela zao wanawekeza pale. Mtu hatakuita show baada ya kuona ile anahisi show kwamba uje alafu vitu vivurugike kwa njia moja ama nyingine…ameniharibia karibu laki tano nimepoteza” Alisema Otile kupitia NTV SASA cha NTV Kenya.

Comments

comments

You may also like ...