Header

Kilichosemwa na Wakili wa Nay wa Mitego baada ya Nay kufikishwa Dar.

Taarifa ambazo zimetufikia jioni ya March 26 ni kuwa staa wa Bongo fleva Nay wa Mitego amefika salama Dar es salaam akiwa chini ya ulinzi wa Polisi ambapo Wakili wake anayeitwa Peter Kibatala ametoa taarifa kwa umma kwa wale waliokua wanataka kujua maendeleo ya Nay baada ya kukamatwa.

Kwenye akaunti yake ya Instagram Peter Kibatala ameandika>>’Nay wa Mitego amefikishwa Central Police Station, Dar es Salaam. Yuko salama na imara; amekula pia. Kwa kuwa amefika jioni sana; hakuna kinachoweza kufanyika leo’

‘Wakili Faraji Mangula @mangulaf1 alifika pale, na kesho tutapigana afikishwe Mahakamani au apewe dhamana,As usual; we never leave a soldier of the struggle behind enemy lines. Tutasimama naye mpaka mwisho,
Viva Nay wa Mitego. Viva freedom’. -Wakili Peter Kibatala.

Comments

comments

You may also like ...