Header

Dkt. Mwakyembe atia neno kuinusuru Serengeti Boys

Waziri wa Mpya wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ameanza kazi katika Wizara mpya kwa pongezi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kuasisi mageuzi ya Kandanda nchini.

Watanzania tumechoka na huu uteja, kusukumwa sukumwa tu kwenye soka.Ni zamu ya watanzania sasa tuonekane katika ulimwengu wa soka”, amesema Waziri Dk. Mwakyembe aliyezungumza na Kamati ya Hamasa kwa Serengeti Boys alipokutana nayo kwa mara ya kwanza jana Machi 20, mwaka huu.

Waziri alikwenda mbali kwa kuiagiza Wizara yake yote ijikite kuhakikisha maandalizi ya Serengeti Boys yanakamilika kwa wakati kwa kusema “Nataka Wizara yangu yote sasa wimbo wetu uwe Serengeti Boys,”

 

Waziri Dkt Mwakyembe aliendelea kusema kuwa michezo ya leo inahitaji uwekezaji hivyo Wizara yake itahakikisha kuwa jukumu hilo analibeba,“Naona kama imechelewa, lakini bado muda upo, tukimbie, nataka Wizara nzima wimbo wetu uwe Serengeti Boys”Alisema kwa hamasa kubwa.

 

Serengeti Boys ipo mjini Bukoba kwa ajili ya mechi yao ya kirafiki dhidi ya Burundi.

Comments

comments

You may also like ...