Header

Simba yajikita kanda ya ziwa kupalilia ubingwa wa VPL

Vinara wa ligi kuu Tanzania Bara Simba Sports Club tayari wameanza safari ya kuelekea kanda ya ziwa wakianzia Kagera ambako watavaana na Kagera Sugar kabla ya kuminyana na Mbao FC  ya jijini Mwanza kwenye mbio za kuusaka ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara .

Simba wanakwenda kucheza na Kagera sugar mjini Bukoba Aprili 2 wakiwa na rekodi ya ushindi wa bao 2-0 walioshinda kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania Bara.

Baada ya mchezo huo wataelekea jijini Mwanza kuumana na Mbao FC Aprili 8 kwenye dimba la CCM kirumba mnamo Aprili 12 watacheza dhidi ya Toto Afrika

Baada ya Simba kumaliza mechi hizo tatu kanda ya ziwa wekundu wa msimbazi watakuwa wamebakiwa na michezo mitatu ya nyumbani  kuelekea kuitimisha mbio za ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara

Comments

comments

You may also like ...