Header

Baghdad aelezea ilivyotokea kutoshiriki kwenye wimbo wa wapo wa Nay wa Mitego

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na mkali wa dundo jipya la ‘Usinipangie’ Baghdad afunguka jinsi alivyoukosa mdundo wa wimbo uliozua makubwa wa msanii Nay wa Mitego na picha lote jinsi ilivyokuwa.

Akizunguma na Planet Bongo ya East Africa Radio Bagdad amesema kuwa mdundo wa ngoma ya wapo ilikuwa autumie kwenye wimbo wake wa ‘usinipangie’ na WAPO lilikuwa liwe wazo la pamoja kwa maana ya kushirikiana kati yake na Nay wa Mitego lakini majukumu ya kazi yalimbana kiasi cha Nay kuufanya wimbo ule pekee yake.

“story behind kuhusu usinipangine ilikuwa nikaifanye studio ya Nay. Siku ambayo naenda studio Moresome alikuwa ameniambia njoo studio kuna mdundo wako ule mdundo wa Nay ndo ilikuwa ni beat yangu…(Nay)akaniambia kama huu mdundo ulikuwa wako basi tuuchangie basi lakini kuna majukumu ya kazi yaliingiliana nikashindwa kufanya hivyo nikamuacha studio” Alisema Bagdad.

 

Comments

comments

You may also like ...