Header

Barakah The Prince aweka wazi kile anachoimba na uhalisia wa maisha yake

Hitmaker wa ngoma ya Acha niende Barakah The Prince ameelezea uhusiano wa malalamiko na minunguniko ya kimashairi ya muziki wake na uhalisia uliopo katika maisha yake ya kimapenzi.

Akizungumzia ukweli wa anachokiimba Barakah amesema kuwa hakuna mahusiano yoyote ya anachokiimba na maisha yake halisi ya kimapenzi bali anafanya muziki wa ajili ya mashabiki na vitu vinavyoendelea kwenye jamii.

“hapana mimi naimba vitu kutokana na vitu vinavyotokea kwenye jamii, mi ujue naimbia mashabiki…kwahiyo hamna hata siku moja kitu ambacho nilishawahi kukiimba kimenikuta lakini ni vitu vinawakuta watu na naviona…kwahiyo naimbaga vitu ambavyo vinauhalisia kabisa na maisha ya kawaida” Alisema Barakah alipkuwa akizungumza na HZB TV.

Hata hivyo Barakah amewashukuru mashabiki wa kusupport kufika kwasababu ya wimbo wake mpya kuwa katika nafasi nzuri katika mtandao wa Youtube.

Comments

comments

You may also like ...