Header

Eric Shigongo atumia kivuli cha Diamond Platnumz kuwachokonoa Mameneja wake

Akutukanae hachagui tusi!!Mtunzi wa vitabu na mmiliki wa kampuni ya Global Publishers Eric Shigongo ametumia mwavuli wa Diamond Platnumz kwa kuwafikishia ujumbe mameneja wake wawili ambao ni Babu Tale na Salaam.

Erick Shigongo ambaye ameanza kwa kusema tangia zamani alikuwa anamfuatilia sana Diamond hata kabla ya kuwa Maarufu hata kwasasa anavutiwa sana na wimbo wake wa Marry You “Nampenda Diamond sana, tena sana (sina uhakika kama analifahamu hili). I am too proud of him! Ni fighter (mpiganaji), from Tandale to Beverly Hills with Neyo kwenye Video ya Wimbo wa Mary You ambao nimemaliza kuuangalia kwenye YouTube hakika si kitu kidogo,Nafahamu kwa sababu nimeanzia chini sana kimaisha. Nikimkumbuka Diamond tangu siku ya kwanza nilipomuona hakika nina kila sababu ya kumuita is the true sign of Tanzania,Bila elimu ya kubwa, bila connection, bila fedha ameweza kuvuka vizingiti vyote hadi hapo alipo. Hakika ni mfano wa kuigwa kwa kila kijana wa nchi hii na duniani kote. BRAVO!“Ameandika Eric Shigongo.

Aliendelea kwa kutoa ushauri kwa Diamond Platnumz na kumwambia kuwa endapo hata sikia ushauri wake basi ataangukia kwenye shimo ambalo lipo mbele yake “LAKINI ninayo machache ya kusema na ninaomba wale wepesi wa kutukana wanivumilie nitoe ushauri wangu kwa Diamond kama mzazi, kaka na Mtanzania mwenzake. Huko ANAKOELEKEA DIAMOND KUNA SHIMO, ASIPORUKA ATATUMBUKIA NA HUO NDIYO UTAKUWA MWISHO WAKE.“Ameandika Eric Shigongo.

Hakuishia hapo aliendelea kutaja sababu za  kuanguka kwenye Shimo kwa Diamond Platnumz kuwa ni watu watatu watakao mdondosha nao ni Nasib Abdul,Babu Tale na Sallam “Kwenye shimo hili Diamond anapelekwa na watu watatu, nao ni NASEEB ABDUL, BABU TALE NA SALAAM. Nimemtaja Naseeb kwa sababu Diamond na Naseeb ni watu wawili tofauti.“Ameandika Eric Shigongo.

Alimaliza kwa kusema sababu zaidi za kuwataja watu hao ataendelea kuzitolea maelezo zaidi kesho kwa kuandika “Nitaendelea kesho.”.Hata hivyo bado jitihada za kuupata upande wa pili kuzungumzia kauli ya Eric Shigongoambayo inaonekana kama ya kichokozi ila jitihada zimegonga mwamba lakini kila kitu tutakujuza kadri ya muda unavyokwenda.

 

 

Comments

comments

You may also like ...