Header

Huu ndiyo ushauri wa Nikki wa Pili kwa BASATA

Msanii kutoka Weusi Kampuni Nikki wa Pili amelitaka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kufanya mpango kuwaita wasanii kwa ujumla ili wakae pamoja waweze kuwaweka sawa juu ya neno “maadili” linalotumiwa kama fimbo ya kuwachapa ‘wasanii’.

Nikki wa Pili amesema kitendo cha kushirikishana kati ya Wasanii na BASATA kitapunguza baadhi ya matatizo kama kufungiwa kazi za Wasanii kiholela bila kumshirikisha au kumpa uhuru Msanii wa kujieleza kama haki ya kila binadamu.

Aidha Nikki alisisitiza kuwa wimbo wao mpya wa ‘Ya Kulevya’ hauhusiano na ishu zozote za kisiasa bali wamemuimbia mwanaume mmoja ambae anapendwa na Familia yake lakini anakuja kuwa msaliti na kuendekeza starehe na baadae kuitelekeza familia.

“Wimbo wetu wa ‘Ya kulevya’ huu ni wimbo wa mapenzi unaozungumza juu ya mwanaume aliyependwa sana na mkewe na familia yake, upendo ukamlevya akaanza kujisahau na kula bata na mwishowe kuharibu familia, tunasikitishwa na watu wanaojaribu kubadili maana hii, imekuwa kawaida kwa msanii kutumia maneno au misemo iliyoko katika jamii wakati huo kwani hata matangazo ya biashara, ‘Comedy’ hufanya hivyo ili kuwavutia wateja wao”Alisema Nikki wa pili kupitia kipindi cha Planet Bongo.

Comments

comments

You may also like ...