Header

Wasafi Dot Com ya Diamond Platnumz yatua Rwanda

Ni hatua kubwa sana kwa wadau na wasanii wa muziki kufanya kila wawezalo ili waweze kunyanyua kipato kutokana na kazi zao, na habari nzuri ni kwamba Wsafi Dot Com platform mpya ya kuuza kazi za wasanii mtandaoni  inayomilikiwa na Diamond Platnumz wamenfungua tawi jipya nchini Rwanda.

Kupitia mitandao ya kijamii Diamond Platnumz amethibitisha kuwa wameingia katika utaratibu wa wasanii na wadau wa muziki nchini Rwanda kufanya biashara ya muziki kupitia Wasafi Dot Com alipoa ambatanisha picha akiwa na muwakilishi wa kampuni itakayosimamia hilo nchin Rwanda.

“Mapema baada ya kukamilisha kikao na Makubaliano na kampuni itayokuwa tawi letu ama agent wa @wasafidotcom nchini RWANDA… Muda si Mwingi nitawatangazia Wasanii wote wa Rwanda ni namna gani mnaweza kuwa na Acount za kuuza nyimbo zenu @wasafidotcom” Alipost Diamond Platnumz.

Comments

comments

You may also like ...