Header

Lil Wayne aja na Young Money Radio

Lil Wayne anaingia kwenye redio. Kupitia Instagram rapper huyo ametangaza ushirikiano na Dash Radio kwa kuanzisha Young Money Radio station.

Weezy amesema kupitia redio hiyo mashabiki wataweza kusikiliza nyimbo exclusive, zake mwenyewe pamoja na wasanii wa Young Money. Episode ya kwanza ya show yake imeruka jana.

“Stoked to announce my new partnership with Dash Radio to present Young Money Radio. Your place to hear everything YM inkludin new musik from me and all my artist. Y’all go tune in. Link in bio. Tomorrow exklusive premiere of @hood2go Kitchen 24 album,” aliandika.

Kwenda kwa Wayne Dash Radio kunakuwa tofauti na wasanii wengi waliochagua kupeleka show zai Beats 1 ya Apple Music wakiwemo Drake, DJ Khaled, Pharrell na Vince Staples.

Comments

comments

You may also like ...