Header

Rick Ross amshindilia Birdman nyundo nyingine

Baada ya kumchana kwenye wimbo ‘Idols Become Rivals’, Rick Ross amemshindilia Birdman nyundo nyingine. Kwenye interview na kituo cha redio cha Atlanta, Hot 107.9, Rozay amesisitiza kutofurahishwa na CEO huyo wa Cash Money Records kwa alichomfanyia Lil Wayne na Dj Khaled.

“I just felt it wasn’t right, you know what I’m saying? Khaled is a great dude,” alisema Ross alipoulizwa kwanini alitoa wimbo Idols Become Rivals.

Rapper huyo amesema licha ya kwamba alimuona Birdman akifanya mambo sio, alichukizwa zaidi kwa kitendo alichomfanyia rafiki yake Khaled.

“If you burn those two [Khaled and Lil Wayne], I already know know how you feel about me, and I just don’t respect it. I just felt like it was time for somebody to let homie know that ain’t gangsta, and you know, you won’t be respected no longer. I won’t let nobody respect you around me,” aliongeza.

Hata hivyo Rozay amesema kuwa wimbo wake haukuwa diss kwa Birdman bali wa kumpa onyo ajiangalie kwa mambo yake anayoyafanya.

Comments

comments

You may also like ...