Header

Ali Kiba na Diamond Platnumz kukaa meza moja

Waziri wa Habari utamaduni sanaa na michezo Dk Harisson Mwakyembe ameingilia kati vita iliyodumu kwa muda mrefu kati ya wasanii maarufu barani Afrika kati ya Nasib Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platnumz na Ali Kiba kwa kuwakutanisha.

Mwakyembe ambae ni waziri mwenye dhamana ya michezo amezungumzia sakata la Diamond na Ali Kiba mbele ya waandishi wa Habari na kuahidi kuwaweka meza moja kama mzazi wao na kuziondoa kabisa tofauti zao.

Nasikia habari kuwa wasanii Diamond na Ali Kiba wanatofauti lakini kwa hili suala la kitaifa nitawaita na kumaliza hili sakata lao na kisha kuhamasisha watanzania kuichangia timu yetu ya Serengeti Boys kuelekea Gabon“Alisema Dk Mwakyembe mbele ya waandishi wa Habari.

Hata hivyo Mwakyembe hakusita kutia neno kwenye mbili za Stars kwa kuibuka washindi huku akimwagia sifa Nahodha wa timu ya taifa Mbwana Samatta.

Comments

comments

You may also like ...