Header

Maua Sama awachoresha wasanii wa Bongo Fleva

Wakati baadhi ya wasanii wakidai kuwa kazi ya muziki hailipi katika kipindi hiki kigumu cha kibiashara, msanii Maua Sama anaetamba na wimbo wake wa ‘Main Chick’ amedai hakuna kitu kinachomuingizia mkwanja mwingi kwa sasa kama muziki mpaka kufikia hatua ya kuagiza gari mpya.

Mrembo huyo amesema kazi yake ya muziki imekuwa ikimfanya aweze kujitegemea katika mambo mengi anayotaka kuyafanya akiachana na elimu aliyoipata akiwa darasani.

“Muziki ni mzuri na ninaupenda sana  ndiyo maana unaona kila nikiimba ninaimba kwa hisia sana. Hii ni kutokana na mimi mwenyewe kuipenda kazi yangu vilevile, muziki unalipa tena sana, mimi umeweza kuniletea mafanikio mengi moja wapo likiwa ni kuagiza gari aina ya ‘IST New Model’ ambalo nategemea hivi karibuni litaingia nchini kutoka nilipoagiza”. Alisema Maua Sama kwenye kipindi cha Planet Bongo.

Aidha Maua amesema ucheshi wake, upole na heshima umemfanya ajione tofauti na wasanii wengine wanaoimba ambao baadhi yao huwa hawaheshimu kazi yao wanayoifanya.

Comments

comments

You may also like ...