Header

Michepuko tupa kule: JB atangaza kuokoka

Muigizaji wa bongo movie  Jacob Stephen ‘JB’ alimaarufu kama Bonge la Bwana amelezea maisha yake halisi ya kiroho na anachokiamini kiiamani.

Akijibu maswali ya mashabiki kupitia Kikangaoni ya Ea Tv JB amesema kuwa ameokoka na anampenda yesu kauli niliyoonesha wazi kuwa anaishi maisha ya uokovu.

“ni kweli nimeokoka na nampenda yesu…usiseme tu nimeokoka…nimeokoka na nampenda yesu kwa kumalizia kama kuna maswali mengine, nina mke mmoja sina hawala wala nyumba ndogo nampenda yesu kristu and i mean it” Alisema JB.

Hata hivyo Jb ni msanii anayeishi maisha na mkewe Irene ambaye kwa muda mrefu hawajafanikiwa kupata watoto na kuwashauri watu walio katika hali kama yao kuvumilia kwakuwa kila jambo anapanga mungu.

Comments

comments

You may also like ...